TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DUCE,ISW,TIE NA JKCI 12-08-2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na.JA.9/259/01/A/359                                                                                                                                            12/08/2023

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kishiriki cha
Elimu Dar es Salaam (DUCE), Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Taasisi ya Elimu
Tanzania (TIE), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) anapenda kuwataarifu
Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe
2023-08-17 hadi 2023-08-19 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi
watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na
sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha
Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za Mwombaji.
vi. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results,
hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips)
HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa
na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja
na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na
kunakili namba ya usaili kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
xiii. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo
mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.
xiv. Msailiwa haruhusiwi kuja na simu au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la
usaili.


Download PDF  Here


 

Share this job